Jamii Wezeshi Foundation · Dar es Salaam

Kuwezesha Jamii Leo, Kujenga Maendeleo ya Kesho.

Tunatoa programu na huduma zinazowasaidia wanawake, vijana na wajasiriamali kupata maarifa, ujuzi na fursa za kuboresha maisha yao.

0Programu za uwezeshaji
0Waanzilishi
0Mwaka wa kuanzishwa
Dares Salaam, Tabata Aroma

Picha

Uwezeshaji kwa Wanawake na Vijana, Oktoba 2026.

Tazama tukio

Walengwa wetu

Tunawahudumia nani?

Wanawake na Vikoba

Wanawake wenye vikundi vya Vikoba/VICOBA, wanaoendesha biashara ndogo au wanaotaka kuanzisha biashara.

Vijana

Vijana wanaotafuta ujuzi wa kujiajiri, wasio na ajira, wenye vipaji vya ubunifu na wanaotaka kuanzisha biashara.

Wajasiriamali

Wajasiriamali wadogo na wa kati, wamiliki wa maduka na biashara za nyumbani, wazalishaji wa bidhaa na watoa huduma.

Namna ya kupata huduma

Hatua sita, kutoka tovuti hadi mafunzo.

  1. 1

    Tembelea tovuti ya taasisi

  2. 2

    Soma maelezo ya programu zinazopatikana

  3. 3

    Chagua programu inayokufaa

  4. 4

    Jaza fomu ya maombi au wasiliana na ofisi

  5. 5

    Pokea maelekezo kuhusu ushiriki, muda wa mafunzo na masharti

  6. 6

    Shiriki programu baada ya kuthibitishiwa nafasi

Ushirikiano

Kikoba Smart: Vikoba bila kumbukumbu za karatasi.

Kupitia Kikoba Smart Digital Support Programme tunahamasisha matumizi ya teknolojia katika usimamizi wa vikundi vya Vikoba.

  • Kupunguza changamoto za kumbukumbu za karatasi
  • Kukuza uwazi katika taarifa za michango na mikopo
  • Kusaidia vikundi kuelewa matumizi ya mifumo ya kidijitali
  • Kuelimisha viongozi na wanachama kuhusu usimamizi wa taarifa za vikundi
  • Kuhamasisha teknolojia katika kufanya maamuzi ya kifedha

Uko tayari kuanza?

Tupigie simu au tutumie WhatsApp, au jaza fomu ya kujiunga. Tutakujulisha hatua inayofuata.