Elimu na mafunzo
Semina, makongamano na mafunzo ya vikundi kuhusu fedha, mikopo, akiba na biashara.
Kuhusu sisi
Jamii Wezeshi Foundation ilianzishwa mwaka 2026 jijini Dar es Salaam ili kuwasaidia wanawake, vijana na wajasiriamali kupata maarifa, ujuzi na fursa za kuboresha maisha yao.
Tulikoanzia
Jamii Wezeshi Foundation ilianzishwa mwaka 2026 na Alfred Bernad Massawe, Richard Bernad Massawe, Evance Ulom na Paul Romanus Amara. Waanzilishi hawa ndio msingi wa taasisi.
Ofisi zetu zipo Tabata Aroma, Dar es Salaam. Programu zetu zinatekelezwa hatua kwa hatua kulingana na rasilimali na uwezo wa taasisi.




Tunachofanya
Semina, makongamano na mafunzo ya vikundi kuhusu fedha, mikopo, akiba na biashara.
Kuanzisha, kusimamia na kukuza biashara ndogo: mpango wa biashara, chapa, masoko na huduma kwa wateja.
Simu janja, mitandao ya kijamii, usalama wa taarifa na mifumo ya kidijitali kama Kikoba Smart kwa vikundi vya Vikoba.
Muundo wa uongozi
Bodi ya Wadhamini inasimamia mwelekeo wa taasisi; Mkurugenzi Mtendaji anasimamia utekelezaji wa shughuli za kila siku. Kwa hatua ya mwanzo taasisi ina timu ndogo na baadhi ya majukumu yanaunganishwa.
Kuongoza usimamizi wa kimkakati na vikao vya bodi.
Kusimamia shughuli za kila siku na utekelezaji wa mipango ya taasisi.
Kuratibu mafunzo, miradi na huduma kwa wanufaika.
Anaripoti kwa Mkurugenzi MtendajiKusimamia tovuti, mifumo ya kidijitali, usalama wa taarifa na usaidizi wa kiteknolojia.
Anaripoti kwa Mkurugenzi MtendajiKusimamia bajeti, kumbukumbu za fedha na shughuli za kiutawala.
Anaripoti kwa Mkurugenzi MtendajiKusimamia mawasiliano, utangazaji, mahusiano na wadau.
Anaripoti kwa Mkurugenzi MtendajiKufuatilia utekelezaji wa programu na kupima matokeo.
Anaripoti kwa Mkurugenzi MtendajiAfisa Ufuatiliaji na Tathmini pia anatoa taarifa za tathmini kwa Bodi inapohitajika.
Tupigie simu au tutumie WhatsApp, au jaza fomu ya kujiunga. Tutakujulisha hatua inayofuata.